Skip to main content

Tanzania: Acheni Kutishia Makundi ya Haki

Mashirika ya Kimataifa yahimiza Kuheshimu Uhuru wa Kujieleza, Kushirikiana

Mashirika yafuatayo pia wameungana, hivi mashirika yanayoidhinisha kwa jumla ni 22. Mashirika: African Women Lawyers Association (AWLA) Nigeria, The Woodhull Freedom Foundation, Planned Parenthood Global, and Defend Defenders/East na Horn of Africa Human Rights Defenders.

Nairobi– Serikali ya Tanzania haina budi kuacha maneno ya chuki dhidi ya vikundi vya asasi za kiraia na kutishia kusitisha kazi zao, asasi 16 zisizokuwa za kiserikali za kitaifa na kimataifa zimesema haya leo. Maneno hayo yamelenga vikundi vinavyosaidia wasichana wajawazito kumaliza elimu yao na vile vinavyofanya kazi kulinda haki za wasagaji, mashoga na waliobadilisha jinsia (LGBT).

Mashirika hayo yalionyesha kukubaliana katika tamko la pamoja la mashirika 25 ya Kitanzania yaliyothibitisha kutoa ushirikiano kwa suala la wanafunzi wenye watoto kurudi shuleni. 

Jacinta, 15, was excluded from school after authorities found out that she was pregnant. She said her teachers took her to a medical clinic to undergo a pregnancy test. She subsequently gave birth prematurely and her baby did not survive. August 5, 2014. © 2014 Marcus Bleasdale/VII for Human Rights Watch

“Rais wa Tanzania na viongozi wengine wa ngazi za juu wana jukumu la kujenga nchi kwa kusaidia kila mmoja kupata na kumaliza elimu na kuondoa ubaguzi,” alisema Elin Martinez, mtafiti wa haki za watoto kutoka Human Rights Watch. “Ulinzi wa haki za watu sio tu unawasaidia wao na familia zao bali unaimarisha taifa zima.”

Matamko ya hivi karibuni ya viongozi wa serikali yanaweza kuathiri shughuli za asasi zinazotajwa, vikundi hivyo vya kimataifa vimesema. Tarehe 22 Juni, 2017, Rais Magufuli alisema, “Katika utawala wangu hakuna mtoto mwenye mimba atakayeruhusiwa kurudi shule.” Alisema kwamba wanafunzi wenye watoto wanaweza kuchagua kufanya mafunzo ya ufundi stadi au kuwa wajasiriamali lakini hawataruhusiwa kuendelea na elimu rasmi katika shule za umma. Katika hotuba hiyo alitoa matamko ya kudhalilisha kuhusiana na mahusiano ya jinsia moja.

Tarehe 25 Juni, Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba alitishia kufuta mashirika ambayo yanapingana na katazo la Rais juu ya wanafunzi wenye mimba na wakina mama vijana kurudi shule na kumshtaki mtu yeyote anaelinda haki za watu wa LGBT.

 
Serikali inakadiria kwamba wasichana 30 kati ya kila 100 waliacha shule kutokana na mimba kwa mwaka 2015. Shule nyingi mara kwa mara hufanya vipimo vya mimba na kufukuza wasichana wanaokutwa na mimba, waliokwisha jifungua au kuolewa na kusababisha safari yao ya masomo kufika ukingoni kabla ya wakati.


Matamko ya hivi karibuni ya Magufuli na Nchemba yanakinzana na juhudi za muda mrefu za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na mashirika ya asasi za kiraia za kuandaa miongozo ya kurudi shule kuhakikisha kwamba wasichana wenye mimba wanaweza kurudi shule baada ya kujifungua. Chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2015 iliweka dhamira ya kuhakikisha kwamba kila msichana ambae anaacha shule kutokana na mimba anaweza kuendelea na masomo.

 


Mwaka 2015, bodi ya wataalam ya haki za watoto ya Umoja wa Mataifa, Kamati ya Haki za Mtoto, ilieleza kuguswa kwake na Tanzania kukosa sheria zilizowazi kuzuia wasichana wenye mimba kufukuzwa shule. Kamati iliitaka serikali ya Tanzania kuchukua hatua za mara moja kuhakikisha muendelezo wa uandikishwaji wa wasichana wanaopata mimba na kuwasaidia katika kujiunga upya na kuendelea na masomo katika shule za umma.

 


Masharti ya Tanzania juu ya haki za watu wa LGBT yana madhara. Katika serikali iliyopita ya Tanzania, wanaume wenye kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja walitambulika kama kundi muhimu katika vita dhidi ya HIV na sera  ya taifa ya HIV inahimiza juu ya juhudi za makusudi kufikia kundi hili. Hata hivyo juhudi hizo zimekoma chini ya serikali ya Magufuli ambayo pia imefanya uvamizi katika taasisi moja inayojishughulisha na masuala ya afya ya wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na kutishia kufunga nyingine.

Mwaka 2016, agizo la Wizara ya Afya lilisamimisha kwa muda “utoaji wa huduma za HIV na AIDS kwa ngazi ya mtaa,” hatua iliyofuatiwa na amri ya kufunga vituo vya kutoa huduma kwa kundi muhimu. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mamlaka za Tanzania zimewakamata na kuwafungulia mashtaka watu dhidi ya makosa yanayohusiana na mapenzi ya jinsia moja na kuwalazimisha kufanya vipimo vya njia ya haja kubwa, hali ambayo ni ya kinyama, isiyokuwa ya kibinadamu na ya kudhalilisha ambayo inaweza kufananishwa na mateso.


Matamko ya serikali yanakinzana na wajibu wa Tanzania kimataifa na kikanda wa haki za binadamu. Wajibu ambao ni pamoja na kuhakikisha kwamba watoto wote wanakwenda shule za msingi na sekondari bila ubaguzi, pamoja na jukumu la kuchukua hatua zote muhimu kuhakikisha wanafunzi wanaopata mimba wanapata nafasi ya kuendelea na masomo yao. Haki ya kupigania haki sawa kwa wote bila ya kujali mwelekeo wa kijinsia na utambulisho wa jinsia inapaswa kulindwa vile vile. Sheria za kimataifa na katiba ya Tanzania zinatambua na kulinda haki ya uhuru wa kujieleza na kushirikiana na wengine. Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu iliiasa serikali kuchukua hatua madhubuti kukomesha ukatili na ubaguzi katika misingi ya muelekeo wa kijinsia na utambulisho wa kijinsia na kutoa maoni yao juu ya uvunjifu wa haki ya uhuru wa kukusanyika kwa amani kwa misingi ya muelekeo wa kijinsia.


Serikali haina budi kusitisha mara moja vitisho dhidi ya kazi na asasi zisizokuwa za kiserikali, vikundi hivyo vimesema. Asasi zote za kiraia inabidi kupewa nafasi ya kufanya kazi bila uoga wa kuadhibiwa kutoka na tafiti zao, utetezi, mipango na huduma muhimu. Tamko la Umoja wa Mataifa la Watetezi wa Haki za Binadamu ambalo Mkutano Mkuu ulilipitisha kwa pamoja mwaka 1998, linatoa maelekezo kwa serikali “kuchukua hatua muhimu na madhubuti kuhakikisha ulinzi kutoka mamlaka husika juu ya [Watetezi wa haki za binadamu] dhidi ya vurugu, vitisho, kulipiza visasi, ubaguzi, shinikizo  au vitendo vyovyote vya makusudi” kama matokeo ya juhudi zao halali za kuchochea haki za binadamu.


“Asasi huru za kiraia zina nafasi kubwa na muhimu katika mijadala, utengenezaji wa sera na huduma katika masuala nyeti yanayoikabili Tanzania,” Michelle Kagari, Naibu Mkurugenzi wa Kanda wa shirika la Amnesty International alisema. “Juhudi za kutishia kuingilia kazi zao na kunyamazisha sauti zao hazina tija na ni kinyume na majukumu ya Tanzania katika sheria za kimataifa.”

Imewekwa sahihi na:
Amnesty International
Center for Health and Gender Equity (CHANGE)

Center for Reproductive Rights
Chapter Four Uganda
Child Rights Information Network
Equal Education Law Centre, South Africa
Global Campaign for Education
Global Observatory for Inclusion
Human Rights Awareness and Promotion Forum (HRAPF), Uganda
Human Rights Watch

 

International Women's Health Coalition
Ipas

 

National Gay & Lesbian Human Rights Commission, Kenya

 

Right to Education Initiative
Robert F. Kennedy Human Rights
Unchained At Last
 

 

 

Your tax deductible gift can help stop human rights violations and save lives around the world.

Region / Country